Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 6 YA 15

Sherehe za utoshelevu wa neema. Moyo wenye kutosheka unaridhishwa na mtoaji na umewekwa huru kutamani karama nyingine.

Dhambi inafanya mambo mawili makubwa kwetu sote. Moja, inatufanya kujichomeka katikati ya ulimwengu, na kuyaathiri maisha yetu wote. Katika misimamo yetu binafsi, wote tunasukumwa sana na matakwa yetu, mahitaji yetu, na hisia zetu, na kwa sababu hiyo, tunakuwa makini sana na kile tusichokuwa nacho kuliko baraka tele ambazo tumepewa. Lakini kuna zaidi; kwa sababu tuna mitizamo yetu, tunageuka kuwa watu wa kulinganisha, tukilinganisha tulivyonavyo na wengine walivyonavyo. N maisha ya kutokutosheka na wivu. Wivu siku zote ni mbinafsi.

Kuna jambo la pili lenye umuhimu sawa ambalo dhambi inatufanyia. Inatufanya kuangalia vitu kwa njia ambayo siyo majibu yanavyopatikana. Kwa hiyo tunaviangalia viumbe ili kupata uzima, tumaini, amani, pumziko, utoshelevu, utambulisho, maana na kusudi, amani ya ndani, na hamasa ya kuendelea. Tatizo ni kwamba hakuna kiumbe kinaweza kukupa yote haya. Viumbe havikuumbwa kutosheleza mioyo yetu. Viumbe viliumbwa kukuonesha kwa yeye aliye na uwezo wa kuutosheleza moyo wako. Watu wengi leo wataamka na kwa njia nyingine wataomba viumbe kuwa mwokozi wao, yaani, kuwapa kitu ambacho ni Mungu pekee awezaye kuwapa.

“Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe. Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.” (‭‭Zab.‬ ‭73:25-26) Haya ni maneno ya mtu aliyejifunza siri ya kujitoa. Unapokuwa umefidhishwa na mtoaji, kwa sababu ndani yake umepata uhai uliokuwa unautaka, unakuwa huru na masumbufu ya utoshelevu yanayowakatisha tamaa uwepo wa watu wengi. Ndiyo, ni kweli kwamba moyo wako utatulia tuu pale utakapopata pumziko Kwake. 

Hapa kuna tunda zuri sana na neema-- moyo uliotosheka, ulijitoa katika kuabudu kuliko kutaka na wenye furaha ya shukurani kuliko mahangaiko ya kuhitaji. Ni neema na neema pekee ambayo inaweza kukufanya uishi kwa amani na kila mmoja wetu. Waweza kupokea neema hiyo leo? 

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/