Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 5 YA 15

Ukiamini kwa miaka elfu moja, hukubaliki zaidi ya wakati ulipoamini mwanzo; kukubaliwa kwako kuna msingi katika haki ya Kristo na siyo yako.

Ukweli ni kwamba dhambi ni janga kubwa kuliko tunavyofikiria na neema ni ya ajabu sana kuliko tunavyoweza kujua. Hakuna ajuaye kikamilifu maandiko yanasemaje kwa ufasaha, kila nyanja ya utu wako ikibadilisha asili ya dhambi angeweza kufikiria kwamba kuna mtu anaweza kuhamasisha ipasavyo na kupanda kiwango cha ukamilifu wa Mungu. Wazo ambalo kila mwanadamu anaweza kufanya ili akubalike na Mungu lazima liwe ni wendawazimu wa hali ya juu. Bado wote tunafikiria kwamba tunwatakatifu kuliko tulivyo, na tunapofikiria hivyo, tunakuwa tumechukua hatua ya kwanza ya kujiona kwamba labda siyo wabaya sana mbele za Mungu.

Na ndiyo maana kuangalia Warumi 3:20 ni muhimu sana. Paulo anaandika, “kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” Kama unaomba wakati wote wa maisha yako, huwezi kuomba maombi ya kutosha kupata kibali kwa Mungu. Kama ulitoa kiasi chote cha fedha kutoka kwenye mshahara wako, huwezi kutoa vya kutosha ili ukubalike na Mungu. Ikiwa kila neno ulilolinena ulilinena ukiwa na ufahamu kamili, huwezi kusema hata ukapata upatanisho na Mungu. Kama ulijitoa kwa wasiovunjika, muda mwingi kwenye huduma, hukuhudumu kiasi cha kutosha kupata kibali cha Mungu. Dhambi ni kubwa sana. Kiwango cha Mungu ni kikubwa sana. Ni kikubwa kuwahi kufikiwa na mwanadamu aliyewahi kupata pumzi yake ya kwanza.

Ndiyo maana Mungu kwa upendo wake alimtuma mwanawe: "“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi". (Rum. 5:8). Unaona, hakukuwa na hakuna njia nyingine. Kuna njia moja tuu ya kukubalika na Mungu--haki ya Kristo. Haki yake imetolewa kwa ajili yetu; wenye dhambi wanakaribishwa katika uwepo wa Mungu mtakatifu msingi ukiwa ni utii kamili. Kristo ni tumaini letu, Kristo ni pumziko letu, Kristo ni amani yetu. Kwa ukamilifu alitimiza matakwa ya Mungu ili kwamba kwa dhambi zetu, udhaifu wetu na kushindwa kwetu, tena tusiogope hasira ya Mungu. Hiki ndiyo neema inafanya! Ndivyo walivyonwatotomwa neema, tunatii kama ibada, siyo kwa jitihada za kufanya lisilowezekana--binafsi tukipata kibali cha Mungu.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/