Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano
Theolojia bora haitaondoa siri katika maisha yako, kwa hiyo pumziko linapatikana katika kumwamini yeye atawalaye, ambaye ni yote, na hana siri.
Sauti yake ilitetemeka asubuhi ile alipokuwa ananiambia nirudi nyumbani haraka. Mke wangu, Luella, ni mwanamke mwenye hisia imara. Hashtushwi kirahisi. Nilijua tunachokabiliana nacho ni kikubwa maana kimemstuwa. Nilikuwa umbali wa masaa sita hivi; nikiwa na msaidizi wangu, nikafanya safari ya wasiwasi kurudi nyumbani.
Nicole, binti yetu, alianza kutembea kurudi nyumbani kutokea kazini jana, kama alivyofanya siku zingine huko nyuma. Gari lililokuwa likiendeshwa na mlevi asiyekuwa na leseni lilitoka barabarani na kumbana Nicole kwenye ukuta. Alikuwa na majeraha makubwa, pamoja na mivunjiko kumi na moja ya nyonga yake na kutokwa na damu nyingi ndani. Nilipofika hospitali na kuingia kwenye chumba cha wagonjwa mahututi cha Nicole, nilifanya kitu ambacho kila baba mwenye tone la damu ya uzazi angefanya. Nilianguka. Nikatambaa mpaka kwenye kitanda cha Nicole, pasipokujua kama ananisikia, na kusema, " Ni mimi baba, hauko peke yako, na Mungu yuko na wewe, pia."
Nilipoingia kwenye chumba kile, ilikuwa kana kwamba dunia nzima iko gizani. moyo wangu ulilia, " kwa nini, kwa nini, kwa nini?" Kama ningetakiwa kuchagua, nisingependa mtoto wetu yeyote apitie kitu hicho. Na kama ningetakiwa kuchagua mtoto mmojawapo, nisingemchagua Nicole katika kipindi kile cha maisha; na theolojia yetu isiyojadiliwa haiukuondoa siri hiyo. Nicole hakupona vizuri, lakini tuliishi miaka minne ya mateso.
Nilishikilia mawazo kwamba maisha yetu yalikuwa hayatabiriki. Tulifarijiwa tena na tena na mawazo kwamba tukiangalia ajali ya Nicole, Mungu hakushangazwa wala hakuogopa. Unaona, hakuna siri kwa Mungu. Huwa hastukizwi.Hajishangaishi jinsi atakavyoshughulika na lisilotarajiwa. Napenda maneno ya Danieli 2:22: " “yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake.”
Mungu yuko pamoja na wewe nyakati za giza kwa sababu hatakuacha. Lakini giza lako si giza kwake. Siri zako si kitu cha siri kwake. Vinavyokushangaza havimshangazi yeye. Anaelewa vyote vinavyokuchanganya sana. Siyo tuu siri zako siyo siri kwake, bali anatawala vyote hata ambavyo ni vy siri kwako.
Kumbuka leo kuna ambaye anaviangalia vile ambavyo kwako ni giza yeye anaona mwanga. Na unapokumbuka kwamba, kumbuka pia, yeye ni tafsiri halisi ya kilicho hekima, chema, kweli, cha kupenda, na uaminifu. Anakutunza wewe na siri zako katika mikono yake yenye utukufu, na kwa sababu hiyo, unaweza kupumzika hata kama kuna giza la siri limeingia mlangoni kwako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.
More