Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 7 YA 15

Kila siku Unamhitaji. Wewe na mimi hatuwezi kuishi bila yeye. Ni nini hicho? Ni uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu.

Sijui nilikuwa wapi wakati ujumbe ulipotoka. Sijui kwa nini nilikosa majadiliano. Siwezi kueleza kwa nini nimekuwa na kukosa ufahamu wa injili. Siwezi kukwambia kwa nini kitu hiki kilikuwa kinakosekana katika muhtasari wangu wa kitheolojia, lakini ilitokea, na ukweli kwa kukosekana huko kulifanya maisha yangu ya kikristo kuwa magumu.

Hapa kulikuwa na theolojia itendayo kazi maishani mwangu kama mtoto wa Mungu. Nilijua kwamba kwa neema nilipata msamaha wa Mungu na kibali cha kuingia umilele, lakini nilifikiri kuanzia sasa na hapo baadaye, kazi yangu ilikuwa ni kukaa tuu. Ilikuwa ni wajibu wangu kuitambua dhambi, kuikataa katika maisha yangu, na kujitoa katika kuishi vizuri zaidi, njia ya kibiblia zaidi. Nilijaribu, niamini; nilijaribu na nikaona haifanyi kazi. Nikaharibu tena na tena. Ilionekana nilishindwa zaidi ya nilivyofanikiwa. Nikazidi kuchanganyikiwa na kukata tamaa. Nilijiona kama nimepangwa kwenye mchezo ambao siwezi kuucheza, na mtu ambaye ni mfungaji mzuri. Nilikumbuka yote haya nilipokuwa chuoni. Ilikuwa saa 12.00 asubuhi, wakati nafanya ibada ambayo sikutaka kufanya, wakati nilipoweka kichwa changu juu ya dawati na kulia, " Siwezi kufanya kitu unachotaka nifanye!" Kisha nikasoma sura inayofuata kwenye masomo ya kila siku ya Biblia, na kwa neema ya Mungu ilikuwa Warumi 8.

Nikarudia sura hiyo tena na tena, pamoja na maneno haya: "“kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.” (Mstari wa 13). Yalikuwa kama fataki zikitoka kichwani mwangu. Mungu alijua mahitaji yangu kama mwenye dhambi yakikuwa makubwa na haingetosha kwa yeye kunisamehe tuu; ilibidi aje na kuishi ndani yangu au nisingekuwa vile nilivyofanywa upya kuwa au kufanya kile ambacho nimezaliwa upya kukifanya.

Ninahitaji uwepo na nguvu ya Roho Mtakatifu aishie ndani yangu kwa sababu dhambi inateka moyo wangu, inapofusha macho yangu, na kudhoofisha magoti yangu. Tatizo langu siyo hukumu ya dhambi tuu; ni kukosa uwezo kwa dhambi pia. Kwa hiyo Mungu huwapa watoto wake kujihukumu, kuona, kutamani, na uwepo wezeshi wa Roho. Siwezi kusema vizuri zaidi ya Paulo mwisho mwa majadiliano yake juu ya karama za Roho: " Huipa uzima miili ya kufa"

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/