Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 12 YA 15

Mungu anakuita kuvumilia kwa imani, na tena, kwa neema, hutulinda na kututunza.

Ni jina la ajabu na la kutia moyo kwa Mungu unayemtumikia, na bado inawezekana kwenye macho yako na akili yako pasipo kuacha kusherehekea utukufu wake. Katika Warumi 15:5, Paulo anamwita Bwana wako " Mungu mwenye saburi". Ukweli huu mdogo unatupeleka kwenye kiini ambapo tumaini lako linapatikana. Ngoja nieleze wazi: tumaini lako halipatikani katika utayari au uwezo wako wa kuvumilia, bali katika ahadi ya Mungu isiyotikisika ya kutokuacha kazi ya neema yake. Tumaini lako ni kwamba umekaribishwa na Yeye ambaye atavumilia hata iweje.

Kwa nini ni muhimu sana kuelewa hili? Kwa sababu saburi yako itaonekana vizuri. Kuna nyakati ambapo utasahau wewe ni nani na unaishi kwa neema ya upendeleo. Kuna nyakati utakatishwa tamaa na kwa kuda utaacha kufanya vitu vizuri ambavyo Mungu amekuita kufanya. Kutakuja nyakati, kubwa na ndogo, ambapo kwa hiari utaasi. Unaweza kuwa unafikiri, " siyo mimi." Lakini fikiria pamoja na mimi--unapokua, kama mkristo, unasema kitu kibaya kwa mtu mwingine, hifanyi hivyo kwa sababu hujui kwamba ni kosa, lakini ni kwa sababu wakati huo hujali kama ni kosa ama la.

Unaona, saburi thabiti inataka hicho, ukamilifu, na kwa kuwa bado hatujafika hapo, lazima tutafute msaada wa tumaini kwingine. Tumaini la saburi yako halipatikani katika tabia yako au nguvu zako, bali katika Bwana. Kwa sababu siku zote ni mwaminifu, unaweza kumtumaini kwamba atakupa unachohitaji kuwa mwaminifu pia. Saburi yako iko kwake, na anaeleza saburi ni ya namna gani! Ni neema ya saburi inayotolewa na Mungu wa saburi inayokupa kila unachohitaji kuendelea kuwa kama alivyokuita na kufanya kati ya sasa na baadaye utakapovuka upande wa pili. Wakati magumu yatakapodhihirisha udhaifu wako na ukomo wa nguvu zako,huna haja ya kutahayari, kwa sababu atakupa saburi hata nyakati hizo wakati unapojisikia huwezi mwenyewe.

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/