YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 1 OF 29

Mungu hujibu maombi. Hufahamu haja zetu hata kabla hatujaomba. Ndiyo maana hutujalia kuyapata hata yale ambayo hatujayaomba. Mungu hutujalia kupata yaliyo mema kutoka kwake wala hawezi kupuuzia tuliyoyaomba kwa jina lake. Sisi wanadamu tulio waovu tunawapa watoto wetu zawadi nzuri. Hakuna mzazi anayeweza kumpa nyoka badala ya samaki au jiwe badala ya mkate mwanawe. Ni hakika kabisa, Mungu aliye Mtakatifu na mwenye wema wote hutujalia kupokea mema zaidi ya yale tunayoomba.

Day 2

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More