Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample
Mungu amemwumba mwanadamu, kwa hiyo anamjua kabisa kimwili na hata kiroho. Hata kabla mtu hajazaliwa, Mungu anajua yatakavyokuwa mambo yote ya maisha yake. Kwa hiyo hata mtoto tumboni mwa mama yake ni mtu aliyeumbwa na Mungu. Ni uhai uliotakaswa na Mungu. Kwa hiyo zaburi hii inatuonyesha enzi ya Mungu, na inamkumbusha pia Mkristo kwamba si mkamilifu. Kwa hiyo tunasisitizwa tumwombe Mungu atuonyeshe dhambi zetu, ili atutakase na kutuongoza katika maisha ya utakatifu.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More