Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample
Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake (m.38). Wakristo na viongozi wa kanisa, je, tumelitendea kazi agizo hili la Yesu? Bila shaka hata katika maeneo unapokaa wewe, ndugu msomaji, kuna watu wengi wanaohitaji huduma ya Mungu na wengi ambao hawamjui Mungu kabisa. Na bila shaka watenda kazi ni wachache mno. Basi, kuanzia leo anza kuomba ombi hili kwa Bwana Yesu. Atafurahi ukifanya hivyo na atafanya umwombavyo. Lakini uwe tayari, maana labda atakupeleka wewe!
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More