YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 23 OF 29

Mmepata bure, toeni bure (m.8). Mitume walikuwa wamepata bure. Yaani hawakumlipa Yesu chochote ili awakubali wawe wafuasi wake na mitume wake. Yesu amewapokea kwa neema na amewaita kwa neema. Ni jambo moja tu lililowastahilisha: Walimpokea Yesu na maneno yake. Ni watu walioitika. Vile vile na wao wasidai chochote kwa watu watakapowahubiria Injili na kuwafanyia huduma yao ya ajabu. Watakaowakaribisha na kuyapokea maneno yao ndio wanaostahili: Nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu(m.13-14). Je, unayatoa bure uliyopokea bure?

Day 22Day 24

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More