YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 25 OF 29

Yesu anasisitiza kwamba tusishangae ikiwa hali ya maisha yetu kama wafuasi itafanana na hali yake mwenyewe. Maana yeye ni mwalimu, sisi ni wanafunzi. Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake? (m.24-25). Yesu anajua maneno haya yanaweza kututia hofu, kwa hiyo anasisitiza mara tatu: Msiogope(m.26, 28, 31). Hata kama watu watajaribu kutulazimisha kulikana jina lake, tusiogope, maana yeye atakuwa pamoja nasi papo hapo na kututia nguvu. Na hata tukiuawa tutashinda tu, maana ajuaye yote na mwenye kuhukumu yuko upande wetu, ni Baba yetu!

Day 24Day 26

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More