YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 21 OF 29

Kwa kadiri ya imani yenu mpate (m.29). Watu waliposikia habari za Yesu wengine walipokea kwa imani, kwa mfano yule bwana mwenye binti aliyekufa (Tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia [Yesu], akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi; m.18) na huyu mwanamke mgonjwa (Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile; m.21-22). Ila wengi hawakuamini tena baadhi yao wakacheka kabisa (m.24: Yesu akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana). Hao vipofu wawili walimwamini. Waliona jambo ambalo wengi wenye kuona hawakuona. Walitambua kwamba ni Kristo, Mwokozi aliyeahidiwa na Mungu. Imani hii walionyesha kwa kumwita Mwana wa Daudi na kwa kuamini uponyaji wake.

Day 20Day 22

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More