YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 9 OF 29

Mungu anafanya kazi kupitia watu. Wayahudi wamevaa magunia na kufunga wakimlilia Mungu, lakini anahitajika mtu wa kwenda kwa mfalme. Esta anasita kwa sababu sheria hazimruhusu, na anahofia maisha yake. Mordekai anasisitiza, Ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo (m.14)? Akiomba ushirika wa Wayahudi, Esta anachukua uamuzi wa ujasiri: Nitaingia kwa mfalme ... nikiangamia, na niangamie (m.17). Hofu gani inakuzuia kuchukua hatua ya ujasiri kwa ajili ya watu wa Mungu?

Scripture

Day 8Day 10

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More