YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 10 OF 29

Mungu amejibu maombi, na Esta anapewa kibali cha mfalme. Mkakati wa Esta ni kuwaokoa Wayahudi, hivyo hababaiki akiruhusiwa kuomba hata nusu ya ufalme. Esta ni mdiplomasia kweli. Hajajidhihirisha, na Hamani hashtuki bali kuona fahari tu. Ila Mordekai anaendelea kuwa kero kubwa kwa Hamani ambaye anaamua kumtundika ili kuondoa udhia. Hivyo mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana humponya nayo yote (Zab 34:19), maana njia zake ni juu sana kuliko njia ya mtu. Mpe Mungu kuamua kuhusu mikakati yako.

Scripture

Day 9Day 11

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More