Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample
Ikiwa nimepata kibali machoni pako, na mfalme akiona vema, nipewe maisha yangu kuwa dua yangu, na watu wangu kuwa haja yangu (m.3). Kwa ombi hili, Esta anajitambulisha kuwa ni Myahudi. Mfalme aghadhibishwa na hila za Hamani, na kuamuru Hamani atundikwe juu ya mti aliomwekea Mordekai. Mungu ni mwaminifu kwa neno lake lisemalo, Hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli (Zab 121:4). Tukiwa watoto wake, tuwe na ujasiri wa kumwomba lolote. Mungu atupenda na kutusikiliza.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More