Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample
Wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni (m.11). Yesu alipoiona imani kubwa kwa mtu ambaye si Mwisraeli, alikumbuka ahadi za Mungu za Agano la Kale, kwa mfano Isa 49:5-6, Bwana asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu); naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia. Ahadi zinatabiri kwamba Kristo hatakuwa Mwokozi kwa ajili ya watu wa Mungu tu (Waisraeli), bali kwa ajili ya ulimwengu mzima! Lengo hili likishafikiwa ndipo Yesu atakuja mara ya pili: Habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja(Mt 24:14). Je, Tanzania nzima imeshafikiwa na Injili?
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More