YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 19 OF 29

Je! umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? (m.29) Agano Jipya linatufundisha kwamba Shetani na malaika zake wana muda mfupi tu:Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi(Rum 16:20). Ndipo watatupwa katika ziwa la moto au jehanamu: Mfalmeatawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake(Mt 25:41). Na huko watateswa milele. Shetani anajua haya. Kwa hiyo ana hasira kubwa:  Shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.... Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele(Ufu 12:12; 20:10). Kuhusu namna ya kutoa mapepo tufuate mfano wa Yesu. Linalohitajika ni neno tu! Neno lenye amri na nguvu: Kulipokuwa jioni, wakamletea [Yesu]wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake. … Akawaambia [wale pepo], Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini (8:16 + 32).  Yesu na wanafunzi wake wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha. Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi. Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii! (Mk 1:21-27) Ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo(Mk 16:17). Nguvu twapata ikiwa maisha yetu yamejaa Neno la Mungu, maombi na toba.

Day 18Day 20

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More