Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample
Esta alipewa nyumba ya Hamani, na Mordekai alichukua cheo cha Hamani. Lakini shida moja kubwa sana ilibaki: Andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme ... hakuna awezaye kulitangua – hata mfalme mwenyewe (m.8). Tena Esta anapata kibali cha mfalme akimwomba. Wayahudi wanapewa haki ya kusimamia maisha yao na kujilipiza kisasi juu ya adui zao siku ileile waliyokusudiwa kuangamizwa. Mungu anapotusamehe dhambi zetu, siyo lazima atuondolee pia madhara yake. Lakini anaweza kutubariki kwa namna nyingine.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More