YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 15 OF 29

Ni vema kufurahi na kupelekeana zawadi tukitokewa na jambo jema kibinafsi au kitaifa. Huzuni aliyokusudia Hamani kwa Wayahudi iligeuzwa kuwa shangwe kutokana na maombi ya Esta kwa mfalme na kuingilia kwa Mungu. Iliamuriwa kusherehekea siku hiyo kila mwaka na kuwakumbuka maskini. Hata leo kuna sikukuu ya Purimu huko Israeli (puri = kupiga kura; kama ilivyoelezwa katika 3:7, Mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani). Linganisha na Pasaka na Krismasi, watu wakipeleka zawadi kwa wagonjwa n.k. Wewe unasherekeaje siku kuu zako na za nchi? Mungu anapewa sehemu gani?

Day 14Day 16

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More