Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample
Mtu asiyefaa, akipata madaraka anaweza kuleta madhara makubwa. Kwa mtu mmoja kutokusujudu na kuinama mbele yake, Hamani anakuwa adui wa taifa zima la Wayahudi, na kutumia nafasi aliyo nayo kutaka kuwaangamiza kabisa. Wakati watu wanafadhaika, mfalme na Hamani wakajiburudisha tu. Watu wangapi wameumizwa ili wakuu watimize azma zao? Jiweke katika nafasi ya Wayahudi, ukisubiri tarehe ya kuangamizwa. Unaelewa kwa nini Mordekai hakuinama? Unakubaliana naye alivyofanya? Uko tayari kufuata mfano wake?
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More