Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample
Kitabu cha Esta kinaonyesha jinsi Mungu anavyotumia matukio ya kawaida kutimiza makusudi yake ya kuokoa watu wake. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti (Mit 14:12). Bila shaka Vashti alikuwa na sababu yake nzuri alipokataa, lakini uamuzi wake ulimgharimu umalkia na kufungua mlango kwa malkia mwingine kuchaguliwa (m.19: Mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria za Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye). Inatupasa tuwe makini tunapofanya maamuzi, hasa katika mazingira yasiyomtukuza Mungu, ili kuepuka matokeo yasiyotarajiwa.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More