Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample
Ishara na maajabu tunayoyaona yakitokea kwa watumishi au huduma mbalimbali, siyo lazima kwamba yote hutokana na Mungu. Lakini Yesu ndiye mwamba imara usiotikisika. Kumwamini Yeye na kutegemea Neno la Mungu katika kila hali, ni sawa na kujenga juu ya mwamba imara usiotikisika. Kufanya kinyume cha hayo na kujenga matumaini kwa wanadamu kwa kutumainia ishara na miujiza tu, ni kama kujenga juu ya mchanga. Majaribu yakija haiwezekani kustahimili, ni kuanguka tu! Hebu jihoji mwenyewe: Wewe umejenga imani yako juu ya nini?
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More