YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/20Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/20

DAY 5 OF 29

Mordekai alipopeleka Esta katika nyumba ya mfalme, alimwagiza asidhihirishe asili yake ya Kiyahudi. Sababu tutaliona baadaye. Esta alipata kibali kwa kunyenyekea kwa wale waliokuwa wanamwandaa mwanamwali atakayekuwa malkia, akapewa mahitaji yake yote. Wao walijua sifa zilizohitajika. Watu wengi wanaacha kuchangamkia fursa na kutoa sababu mbalimbali, badala ya kunyenyekea na kumtegemea Mungu na kuacha matokeo mkononi mwake. Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? (Rum 8:31)

Scripture

Day 4Day 6

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More