Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Daudi anaratibu ibada, iongozwe na Walawi fulani. Zaburi wanayoimba hufanana na Zab 96 na 105:1-15. Ziliimbwa wakati wa matukio makubwa kama hili. Wanamwabudu Mungu, wakimsifu kwa uaminifu wake kwa agano alilofanya na Ibrahimu ambalo lilikuwa kazi ya Mungu. Katika mataifa yote alimchagua Ibrahimu, akamwahidi kumfanya kuwa taifa kubwa na kuwapa Kanaani iwe nchi yao. Mwanzoni walipokuwa wachache, wangeliweza kuangamizwa na maadui kwa urahisi, lakini Mungu aliwahifadhi kwa njia ya miujiza.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz