Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Kwa kutazama mambo yote ambayo Mungu aliwatendea, watu wake walihamasishwa kumsifu na kutangaza matendo yake makuu kwa mataifa yote. Hata uumbaji wote unaambiwa kujiunga na hao wanaomwimbia Mungu na kumsifu. Huruma yake isiyokuwa na upungufu iliwavuta Waisraeli kumtegemea Mungu siku zote ili awaokoe. Kuanzia siku hiyo ibada za kila siku ziliendelea mbele ya sanduku la agano huko Yerusalemu. Katika m.23-24 imeandikwa:Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. Itikio lako likoje? Wasiomwamini Bwana bado wapo. Unawashuhudia juu wokovu wa Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz