Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Daudi aliwashinda Wafilisti magharibi, adui asilia wa Israeli, Wamoabu mashariki, Washami kaskazini, na Waedomu kusini. Hawa ndio maadui wakuu wa Israeli waliowazunguka. Ushindi pia uliwezesha kukusanya nyara ambazo zingekuja kutumika kama vifaa vya kujengea hekalu. Ushindi wote unaoneshwa kuwa si ushindi wa Daudi bali wa Mungu. Tafakari ulivyoandikwa katika m.6 na 13:Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda. ... Akaweka ngome katika Edomu; na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda, kila alikokwenda. Daudi alifanywa mfalme mwenye kuwahukumu kwa haki watu wake wote. Mpendwa, unavyowajibika kwa nafasi yako ya kila siku, je, inaonesha uwepo wa Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz