Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Waisraeli walishambulia miji ya Waamoni na kushinda tena na tena katika vita dhidi ya Wafilisti.Haya siyo tu mapambano kati ya majeshi, au mtu na mtu, bali ni vita kati ya miungu. Mungu pekee aliye hai anawapa ushindi waamini wake. Kama dalili yake, Daudi anavishwa taji ya Milkomu, mungu wa Waamoni (ndivyo yasemavyo maandiko ya awali ya Kiebrania). Hii itutie moyo kuwa tutashinda juu ya shetani! Yesu anasema,Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu(Yn 16:33b).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz