Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Baada ya kuhamisha hema la kukutania Yerusalemu,Daudi aliamua ajenge makao ya kudumu kwa sanduku la agano, yaani nyumba ya Mungu. Ila Mungu anamwambia kuwa kipindi cha kujenga hekalu bado hakijatimia. Daudi hastahili kulijenga. Ndivyo Daudi mwenyewe anavyomwambia mwana wake, Sulemani, katika 1 Nya 22:8,Neno la Bwana likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu. Badala yake, Bwana atamjengea Daudi “nyumba” (m.11). Maana yake, katika ukoo wa Daudi atazaliwa “mwana wa Daudi” ambaye atatawala milele juu ya ufalme wa Mungu. Ni unabii kuhusu Yesu.Yeye ndiye atakayenijengea nyumba(m.12).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz