Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Mungu analeta pigo linaloua watu sabini elfu. Daudi anapomwona malaika wa Bwana anayetekeleza adhabu ya Mungu, anapokea lawama zote kwa makosa yake, akiomba wasipigwe watu wasio na hatia, bali yeye mwenyewe. Ndipo Mungu anaghairi. Maana yake, Daudi anaambiwa ajenge madhabahu mahali alipofikia huyo malaika, na amtolee Mungu dhabihu. Mungu anaipokea kwa moto ushukao kutoka mbinguni, hatia ya Daudi ikaondolewa, na pigo likasimamishwa. Itikio la Daudi ni shukrani na hofu.Daudi alipoona ya kwamba Bwana amemwitikia katika kiwanja cha Arauna, Myebusi, ndipo hutoa dhabihu huko. ... Wala Daudi hakuweza kwenda mbele yake ili kumwuliza Mungu; kwa sababu aliona hofu kwa ajili ya upanga wa yule malaika wa Bwana(m.28 na 30).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz