Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Baada ya miezi mitatu (13:14) Daudi alikuwa ameandaa mahali pa kufaa pa kuhifadhia sanduku. Wakati anafanya haya Daudi anagundua kuwa wanaotakiwa kulibeba sanduku ni Walawi tu. Kwa hiyo anawaagiza makuhani na Walawi wajitakase, kisha walibebe sanduku. Kwa ajili ya tukio hili, waimbaji na wapiga vyombo miongoni mwa Walawi waandae muziki utakaoendana na furaha kubwa ya kupandisha sanduku la Bwana hadi mahali pake. Daudi anatufundisha kuwa na maandalizi mazuri kabla ya ibada zetu.
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz