Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

SIKU 11 YA 31

“Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, maana Mungu ndiye aliye ngome yangu”(m. 17). Zaburi hii huonyesha usujudiaji mkubwa. Ina udhihirisho mkubwa wa moyo uliojaa ibada ya kweli kwa Mungu. Ni Mungu pekee anayepaswa kuabudiwa, kwa msingi wa kile kimfanyacho kuwa vile alivyo katika asili yake. Ila haitoshi kuishia hapo. Mungu anastahili kusifiwa kwa mambo makubwa anayofanya kwa watu wake. Rudia m.16-17 ukifanya maneno haya kuwa maombi yako leo. Ongeza tu mifano ya Mungu alivyokuwa ngome yako.“Nitaziimba nguvu zako asubuhi[mifano yako], nitaziimba fadhili zako kwa furaha[mifano yako]. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, na makimbilio siku ya shida yangu [mifano yako]. Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu[mifano yako]”.

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz