Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Aliye heri ni mtu anayefahamu mahali pa kukimbilia wakati wa mtafaruku. Daudi alifahamu pa kugeukia. Ni kwa Mungu. Kwa hiyo anaanza kwa ombi la kupata msaada. Mara mbili anamwomba Mungu, “Uniponye”; na pia anasihii,“Uniokoe”(m.1-2). Anajiona yuko kwenye hatari toka wale anaowaeleza kama “watu wa damu”(m. 12). Mapokeo ya zamani husema hao ni watu waliotumwa na Sauli ili wamwue Daudi. Duniani tunaishi katika misukosuko mingi ya maisha. Tumwombe Mungu. Ndiye awezaye kutuokoa. Kumbuka ilivyoandikwa katika Zab 55:22: “Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz