Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Neno la Mungu huenda moja kwa moja kwa mlengwa. Mfalme anayeumwa anajulishwa kuhusu kifo chake. Anapewa ujumbe wa kutengeneza maisha na nyumba yake. Nyumba inahusu wote wakaao nyumbani. Hezekia hapotezi nafasi na wakati. Anamgeukia Mungu. Ombi lake linakubaliwa. Anaruzukiwa siku za kuishi miaka 15. Kwa njia ya maombi Mungu anaweza kuigeuza hali yetu. Usisite kumwomba Mungu abadilishe maisha yako. Kwa mfano tunasoma hivi katika 2 Nya 32:24-26:Hezekia akaugua akawa katika hatari ya kufa; akamwomba Bwana; naye akasema naye, akampa ishara. Walakini kadiri alivyofadhiliwa Hezekia hakumrudishia vivyo; kwa kuwa moyo wake ulitukuka; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu. Hata hivyo Hezekia akajinyenyekeza kwa ajili ya huku kutukuka kwa moyo wake, yeye na wenyeji wa Yerusalemu, hata haikuwajia hasira ya Bwana siku za Hezekia. Acha kiburi kinachokusumbua wewe na wenzako, na jinyenyekeze kwa Mwokozi wako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz