Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Ni maelezo juu ya utawala wa Sauli ulivyomalizika. Kifo chake ni hukumu ya Mungu juu ya Sauli, kwa sababu hakuwa mwaminifu na mtii kwake. Kwenda kwa mwenye pepo wa utambuzi ni mfano tu wa tabia yake ya kutokuwa mwaminifu inayojionesha katika utawala wake wote. Kifo cha kujiua ni njia ya kuepuka aibu mbele ya watu, lakini si mbele za Mungu. Kwa Wakristo, tumwendee Yesu aliyekubali kuchukua masikitiko na aibu yetu, hata kufa msalabani kwa wokovu wetu; kama ilivyoandikwa katika Isa 53:5:Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Yesu ametuondolea aibu zetu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz