Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Daudi alijua kuwa udhaifu wa Israeli ulitokana na ukosefu wa nia ya Sauli kumhusu Mungu. Hata sanduku la agano, mfano wa uwepo wa Mungu, lilikuwa limesahauliwa. Daudi alilileta Yerusalemu mahali panapostahili, katikati ya maisha ya kidini ya taifa. Mpango huu ulipata pigo kwa kukosekana kwa heshima kwa sanduku hilo. Kama tokeo lake,Daudi akamwogopa Mungu siku ile, akasema, Nitajileteaje sanduku la Mungu kwangu?(m.12). Kwa hiyo Daudi alielekeza sanduku likae kwa muda nyumbani mwa Obed-Edomu aliyeishi Gathi; kuwepo kwa sanduku nyumbani kwake kulileta baraka. Jipime: Ikoje na hofu yako kwa Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz