Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Askari na majemadari wa makabila ya Israeli walijiunga na Daudi kwa hiari yao ili kumsaidia katika kuujenga na kuuimarisha ufalme wa Israeli. Makundi ya kijeshi walitumwa huko Hebroni wakiwa na wajumbe wao waliojikabidhi kwa Daudi, awe mfalme wao mpya. Mpendwa, ushindi wa Yesu dhidi ya dhambi, kifo na shetani ni dhahiri. Amua kujiunga naye akushindie maadui hawa, na akupe uzima wa milele. Zingatia jinsi furaha ya kuwa na kiongozi hodari ilivyoleta ukarimu mkubwa:Wakaleta chakula juu ya punda, na ngamia, na nyumbu, na ng'ombe, vyakula vya unga, mikate ya tini, na vichala vya zabibu kavu, na divai, na mafuta, na ng'ombe, na kondoo tele; kwa kuwa kulikuwa na furaha katika Israeli(m.40).
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz