Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Kazi kubwa ambayo mashujaa wa Daudi walifanya ni kuimarisha na kulinda ufalme wa Israeli. Na mashujaa hao waliongozwa na watu watatu ambao wawili wametajwa: Yashobeamu na Eleazari (wa tatu aliitwaShama, mwana wa Agee, Mharari; 2 Sam 23:11). Hawa walihatarisha maisha yao kwa ajili ya mfalme Daudi na Israeli yote. Huu ndio wajibu wa askari wa Yesu tulio nao, kuwa mwaminifu katika hali zote - hata kufa kwa ajili yake. Paulo anafafanua hili katika Flp 1:21,Kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz