Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Uimarishaji wa utawala wa Daudi juu ya Israeli huko Yerusalemu unaanza. Wazee wa Israeli wamtawaza Daudi kwa sababu mbili: 1. Mungu amemteua. Kama Israeli wote walivyomwambia Daudi:Bwana, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli(m.2b). 2. Daudi ameshajitambulisha kama kiongozi mzuri. Kama Israeli wote walivyomwambia Daudi:Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli(m.2a). Kuinuliwa kwa Daudi hakukumfanya kumsahau Mungu. Hivyo hufanana ya Yesu katika Yn 12:32, akisema,Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.Kama tokeo kubwa la utawala wao, Daudi na Yesu wote wawili walileta umoja. Kuhusu Daudi imeandikwa katika m.1 kwambaIsraeli wote wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.Na Yesu anasema hivi katika Yn 17:22:Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.Mpendwa, unapoinuliwa, utukufu ni wa nani?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz