Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

SIKU 14 YA 31

Hezekia alipokwisha kuponywa na kuokolewa alijibu kwa kushuhudia. Alijua kuwa maombi yake yameleta msamaha na ukombozi. Kabla ya hapo hakujua baraka wapewayo wanaomtegemea Mungu (Isa 57:1-2,Mwenye haki hupotea, wala hakuna atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya. Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake). Anatambua kuwa Mungu ameyahifadhi maisha yake. Hivyo anamtukuza Mwokozi! Uwapo katikati ya hatari ya kifo, umtegemee Yesu. Furaha ya anayemtegemea Mungu inaonekana katika uwezo wa Mungu anayeokoa. Katikati ya hatari kuna nuru mpya. Yesu anaokoa kwa kuziondoa dhambi zetu. Daima udumu ukimtegemea Mungu.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2025

Soma Biblia Kila Siku 03/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko, 1 Nyakati na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz