Zab 59:1-9
Zab 59:1-9 SUV
Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, Uniinue juu yao wanaoshindana nami. Uniponye nao wafanyao maovu, Uniokoe na watu wa damu. Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamenikusanyikia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu. Bila kosa langu huenda mbio, hujiweka tayari; Uamke uonane nami, na kutazama. Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uamke. Uwapatilize mataifa yote; Usiwarehemu waovu wafanyao uovu hata mmoja. Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa, Na kuzunguka-zunguka mjini. Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye? Na Wewe, BWANA, utawacheka, Utawadhihaki mataifa yote. Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu