Zaburi 59:1-9
Zaburi 59:1-9 BHN
Ee Mungu wangu, uniokoe na maadui zangu; unikinge na hao wanaonishambulia. Uniokoe na hao wanaotenda maovu; unisalimishe kutoka kwa hao wauaji! Tazama! Wananivizia waniue; watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu. Bila ya kosa, hatia au dhambi yangu, wanakimbia, ee Mwenyezi-Mungu, kujiweka tayari. Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukatazame na kunisaidia! Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu Mwenye Nguvu, Mungu wa Israeli. Uamke, uwaadhibu hao watu wasiokujua; usiwaache hao wanaopanga ubaya. Kila jioni maadui hao hurudi wakibweka kama mbwa, na kuzungukazunguka mjini. Tazama, ni matusi tu yatokayo mdomoni mwao, maneno yao yanakata kama upanga mkali; tena wanafikiri hakuna anayewasikia. Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawacheka; unawapuuza hao watu wote wasiokujua. Nitakungoja, ewe uliye nguvu yangu; maana wewe, ee Mungu, u ngome yangu.