Zab 59:10-17
Zab 59:10-17 SUV
Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu. Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau; Uwatawanye kwa uweza wako, Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu. Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao. Uwakomeshe kwa hasira, Uwakomeshe watoweke, Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo, Na hata miisho ya dunia. Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa, Na kuzunguka-zunguka mjini. Watatanga-tanga hao wakitafuta chakula; Wasiposhiba watakesha usiku kucha. Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu. Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.