Zaburi 59:10-17
Zaburi 59:10-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu. Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau; Uwatawanye kwa uweza wako, Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu. Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao. Uwakomeshe kwa hasira, Uwakomeshe watoweke, Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo, Na hata miisho ya dunia. Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa, Na kuzunguka-zunguka mjini. Watatanga-tanga hao wakitafuta chakula; Wasiposhiba watakesha usiku kucha. Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu. Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.
Zaburi 59:10-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu wangu utanijia na fadhili zako, utaniwezesha kuwaona maadui zangu wameshindwa. Usiwaue mara moja, watu wangu wasije wakasahau; ila uwayumbishe kwa nguvu yako, uwaporomoshe chini. Ee Bwana, wewe ndiwe ngao yetu! Wao hutenda dhambi kwa yote wasemayo, kwa hiyo na wanaswe katika kiburi chao! Kwa sababu ya laana na uongo wao, uwateketeze kwa hasira yako, uwateketeze wasiwepo tena; ili watu wote wajue kuwa wewe ee Mungu watawala wazawa wa Yakobo hata mpaka miisho ya dunia. Kila jioni maadui hao hurudi wakibweka kama mbwa, na kuzungukazunguka mjini. Hupitapita huko na huko wakitafuta mlo, na wasipotoshelezwa hunguruma. Lakini mimi nitaimba sifa za nguvu yako; nitashangilia asubuhi juu ya fadhili zako; maana wewe umekuwa ngome yangu na kimbilio langu wakati wa taabu. Ewe uliye nguvu yangu, nitakuimbia sifa; ee Mungu, wewe u ngome yangu; Mungu mwenye kunifadhili!
Zaburi 59:10-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kutazama kwa ushindi juu ya adui zangu. Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau; Uwatawanye kwa uweza wako, Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu. Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao. Uwakomeshe kwa hasira, Uwakomeshe watoweke, Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo, Na hata miisho ya dunia. Wakati wa jioni hurudi, wakilia kama mbwa, Na kuzungukazunguka mjini. Wanatangatanga wakitafuta chakula; Na kunung'unika wasiposhiba. Nami nitaimba juu ya nguvu zako, Nitaimba kwa furaha juu ya fadhili zako asubuhi. Maana umekuwa ngome yangu, na kimbilio wakati wa mateso yangu. Ee nguvu zangu, nitakuimbia sifa, Maana Ewe Mungu ndiwe ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.
Zaburi 59:10-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu. Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau; Uwatawanye kwa uweza wako, Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu. Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao. Uwakomeshe kwa hasira, Uwakomeshe watoweke, Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo, Na hata miisho ya dunia. Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa, Na kuzunguka-zunguka mjini. Watatanga-tanga hao wakitafuta chakula; Wasiposhiba watakesha usiku kucha. Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu. Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.
Zaburi 59:10-17 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mungu wangu unayenipenda. Mungu atanitangulia, naye atanifanya niwachekelee wale wanaonisingizia. Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu, au sivyo watu wangu watasahau. Katika uwezo wako wafanye watangetange na uwashushe chini. Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao, kwa ajili ya maneno ya midomo yao, waache wanaswe katika kiburi chao. Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka, wateketeze katika ghadhabu, wateketeze hadi wasiwepo tena. Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia kwamba Mungu anatawala katika Yakobo. Hurudi jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji. Wanatangatanga wakitafuta chakula, wasipotosheka hubweka kama mbwa. Lakini mimi nitaziimba nguvu zako, asubuhi nitaimba kuhusu upendo wako; kwa maana wewe ndiwe ngome yangu na kimbilio langu wakati wa shida. Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa. Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, Mungu unayenipenda.