Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano
Hapa pana tofauti kati ya Petro na Yuda jinsi walivyoishughulikia dhambi. Petro alipotambua dhambi yake, alipondeka, akajuta na kutubu. Bali Yuda alitafuta tu kujihalalisha mwenyewe kwa kutenda aliyofikiri kuwa ni mema bila kutubu. Kutotubu hufanya dhambi ibaki bila kuondolewa. Madhara ya dhambi yalimpelekea kujiua. Baba yetu Adamu alipotenda dhambi, matokeo yake yalikuwa makubwa. Kizazi chake chote kikawa chini ya laana ya dhambi hiyo hadi leo. Kumbuka kutubu kila utambuapo dhambi. Yesu anasamehe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz