Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 10 YA 30

Matendo yote ya dhihaka aliyotendewa Yesu katika kuuawa kwake yalikuwa kinyume na jinsi Yesu alivyo katika uhalisi wake. Walifanya yote kwa kumsuta, lakini Yeye ataonekana katika enzi yake kuu kama Mhukumu mwenye haki, Mfalme na Mtawala. Walimchanganya na wahalifu, lakini kumbe Yeye ni Mtakatifu, na tutamwona katika utukufu wa utakatifu wake. Walimshutumu kama asiyeweza kujiokoa, kumbe alifufuka kwa uweza, akawa mshindi wa mwiba wa mauti na udhalimu wote. Kwake kila goti litapigwa.

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana