Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 11 YA 30

Mshahara wa dhambi ni mauti. Kifo cha Yesu hueleza kuwa ghadhabu ya Mungu imepitia na dhambi imepatilizwa. Saa ya kufa kwa Yesu msalabani, Mungu alizuia msaada wake kwa mwana wake mpendwa, ili alipe gharama kamili ya dhambi zetu kwa kufa kwake. Pazia la hekalu lililotenga watu na Patakatifu pa Patakatifu, lilipasuka kuonyesha kuwa sasa deni la dhambi halipo tena, na twaweza kwenda mbele za Mungu bila kuhitaji kuleta malipo mengine. Sote tunawiwa kumshukuru Mungu kwa wokovu mkuu jinsi hii.

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana