Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 7 YA 30

Petro na upendo wake kwa Yesu umeingia majaribuni. Kwa woga wa kujumuishwa kwenye mashtaka ya Yesu, anamkana Bwana wake. Yesu anavyomwambia Petro katika Mt 26:34 inatimia:Amin, nakuambia wewe, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu. Pengine wengi wetu tungefanya hivyo na zaidi, pengine hata kuacha kabisa Ukristo. Petro alikuwa mtu dhaifu kama sisi. Lakini ijapokuwa alimkana Bwana wake, twaona mara moja kujuta kwake na kuomba msamaha alipolia kwa majonzi. Na Bwana alimsamehe. Inawezekana sisi nasi tunamkana Bwana mara kwa mara. Tumkimbilie Yesu tukijutia hali hiyo na kutubu.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana