Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Fungua Milango. Fungua Mioyo.Mfano

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

SIKU 8 YA 8

Mtindo wa maisha.

Mungu huwajali watu wake kupitia kwa watu wake.

Katika mfululizo huu, tumetafakari mifano kadhaa ya ukarimu iliyopatikana ndani ya Biblia na mwito wa kusambaza ukarimu bila ya manung’uniko na kwa ukarimu, sio tu kwa wageni wetu bali vile vile kwa watakatifu na kwa watu tusiowajua.

Kama waamini na sehemu ya Mwili wa Kristo, tunadhihirisha kufanana na Kristo na upendo wa Mungu tunapotoa ukarimu. Fikiria kuhusu dunia ambayo sisi sote tumejitoa kufungua milango yetu, kuwaheshimu wengine kuliko sisi wenyewe na kushirikishana mmoja na mwingine!

Ukarimu ni zaidi ya zoezi la nyakati fulani, ni njia ya kuishi. Warumi 12:9-21 inafafanua sifa za ukarimu wa Kikristo. Unahitaji muda wetu, fedha, ujuzi na rasilimali nyingine tushirikishane na wengine kwa wema na kwa heshima. Unadai kujitoa sadaka. Ni upendo katika matendo.

Maandiko yanatwambia kwamba Yesu, wanafunzi wake na manabii walikaribishwa katika nyumba nyingi kwa upendo, heshima na kwa wema wa zaidi ya kawaida.

Martha na Mariamu walitoa ukarimu kwa Yesu (Luka 10:38-42). Prisila na Akila walimkaribisha Paulo (Matendo 18:2-3). Sara na Ibrahimu walionyesha ukarimu kwa wageni wao (Mwanzo 18:1-8). Tabitha alionyesha wema kupitia kwa matendo yake (Matendo 9:36), na Boazi alionyesha ukarimu wa kipekee na wema kwa Ruthu (Ruthu 2:8-16). Orodha inaendelea.

Biblia ndiyo msingi wa maisha ya Kikristo, na kutokana na wingi wa mifano tunayoshirikishwa katika Neno la Mungu, tunaweza kujifunza kwamba kufanya ukarimu maana yake ni kuwakubali watu, kushirikishana nao, kukabiliana na mahitaji yao sawa na huruma ya Mungu, na kuwatendea kwa heshima.

Tunamtukuza Mungu kwa ajili ya Jeshi la Wokovu (Kanisa), wanaotenda ukarimu kwa mikono ya ukarimu kati ya wale wenye uhitaji, jamii zinazoteseka na wakimbizi. Na yote ni kuleta utukufu, heshima na sifa kwa Mungu ili watu wafahamu neema iokoayo ya Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Hili lazima liwe ndilo lengo letu la mwisho.

Mtu binafsi anaweza kuuishi ukarimu na wengine katika familia zetu, sehemu za kazi na katika jamii, na bila shaka Kanisani. Lakini hebu tusijaribu kamwe kufanya hivyo sisi wenyewe. Tumtegemee Mungu, Mwanae Yesu Kristo na uwezo wa Roho Mtakatifu tunavyofungua milango yetu na mioyo yetu kwa wengine kwa upendo.

Kutafakari:

Je, sisi kwa kweli tunatenda ukarimu kwa upendo, huruma, na kwa ukarimu, au tunapitia tu katika mwendo bila ya makusudi ya moyoni?

Maombi:

Mpendwa Baba wa Mbinguni, katika huruma na upendo wako, twaomba tutoe ukarimu kwa wote, kwa utukufu na heshima yako na kwa kusudi la Ufalme wako, katika uwezo wa Roho Mtakatifu. Katika Jina la Yesu. Amina.

siku 7

Kuhusu Mpango huu

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

Tukiwa na milango iliyofunguliwa na mioyo iliyofunguliwa, tunaweza kuwakaribisha wengine mahali watakapoonekana, wanapopendwa na pale wanapothaminiwa. Katika mfululizo huu wa siku nane, tunakualika uangalie kwa karibu mifano na hadithi za ukarimu zinazopatikana katika Biblia na uwe na muda wa kutafakari jinsi wewe unavyoweza kufanya ukarimu vizuri kwa kutumia maisha yako mwenyewe.

More

Tungependa kumshukuru Salvation Army kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org

Mipango inayo husiana