Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Fungua Milango. Fungua Mioyo.Mfano

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

SIKU 7 YA 8

Kuonyesha ukarimu.

Mgeni katika mazingira ya Kiafriika hukaribishwa wakati wowote hata bila ya taarifa ya mapema. Methali ya Washona wa Zimbabwe, ‘muenihaapedzi dura’ maana yake ‘mgeni hamalizi akiba yako’. Hii huangazia ukweli kwamba kuwashirikisha wengine kile ulicho nacho, pamoja na mgeni au mgeni ambaye hakukaribishwa, hakutasababisha wewe upate hasara kubwa. Methali ya Kinyarwanda, ‘Umushyitsiakurishaimbuto’, maana yake ‘mgeni hukufanya upike mbegu ulizohifadhi kwa ajili ya kupanda’. Unapotumia rasilimali zako bora sana na zenye thamani kwa kuwatumikia wageni, wewe vile vile hupata nafasi ya kuzifurahia hizo rasilimali maalum.

Katika Luka 10:38-42, tunasoma hadithi ya Yesu nyumbani kwa Martha na Mariamu, hadithi inayozungumzia ukarimu kama unavyoeleweka katika dhana ya Kiafrika. Yesu alikuwa njiani na akaamua kuingia katika nyumba ya Martha na Mariamu bila ya mpango wa mapema, hata hivyo ukaribisho wa ukarimu bado ulitolewa. Hii inatudhihirishia kwamba ukarimu usitegemee wingi wa rasilimali zetu bali utegemee mahitaji ya wale tunaowakaribisha. Ukarimu, katika hali hii, unakwenda zaidi ya kutoa chakula tu; unaonyesha utayari wa kujali, kusaidia, kukaribisha, na kuwepo.

Katika dunia, wapo wengine ambao wana vitu zaidi vya kuwagawia wengine, lakini bado hawako tayari kuachana na vile walivyo navyo. Wapo wengine ambao wana vitu vya kutosha tu lakini wanapata shida kuwaalika wengine waje washirikishane. Iwe tuna ghala imejaa rasilimali, tuna kidogo tu kilichobakia kabatini, tunaitwa tufungue milango yetu na tuwakaribishe wageni kwa njia yoyote. Yesu anatuita tuwepo kutumika, hata wakati tukijisikia hatujajiandaa au tuna rasilimali kidogo. Anatutaka tutoe kwa wengine wakati kuna hitaji, sio tu wakati inawezekana au inapotupendeza sisi.

Ukarimu wa kweli unatokea kwenye moyo mkarimu na upendo unaojali unaotaka mema kwa wote, pamoja na kwa wageni.

Kwa ajili ya kutafakari:

Kutafakari hadithi hii fupi, nini huhamasisha matendo yako ya ukarimu leo?

Je, ukarimu wako hudhihirisha utayari wako, na uwepo wako kuwatumikia wengine bila ya mipaka?

Maombi kwa ajili ya leo:

Mpendwa Bwana, ninapowafikiria wale ambao wanaweza kuonekana mlangoni kwangu bila taarifa, nisaidie kuwaonyesha aina ya ukarimu ambao unatoka moyoni...unaosambaza upendo na kujali na wa hamu ya kuwakaribisha kama dhihirisho la upendo na neema yako isiyo na mipaka. Amina.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

Tukiwa na milango iliyofunguliwa na mioyo iliyofunguliwa, tunaweza kuwakaribisha wengine mahali watakapoonekana, wanapopendwa na pale wanapothaminiwa. Katika mfululizo huu wa siku nane, tunakualika uangalie kwa karibu mifano na hadithi za ukarimu zinazopatikana katika Biblia na uwe na muda wa kutafakari jinsi wewe unavyoweza kufanya ukarimu vizuri kwa kutumia maisha yako mwenyewe.

More

Tungependa kumshukuru Salvation Army kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org

Mipango inayo husiana