Fungua Milango. Fungua Mioyo.Mfano
Mtiririko wa neema.
Naona jinsi waandishi wa injili wanavyoelezea mwingiliano wa Yesu na Wasamaria kuwa unalazimisha bila kikomo. Bila shaka, alivyokuwa anakua huko Nazareti, inawezekana Yesu alikutana na upendeleo na ubaguzi wa jamii yake dhidi ya majirani zao. Wayahudi na Wasamaria walikuwa na malalamiko mmoja kwa mwingine yaliyotoka nyuma karne nyingi. Uhasama, tofauti za kidini na misimamo ya kisiasa iliwatenganisha na mara kadhaa iliwaka ikawa vurugu.
Inaeleza, kwamba tunapoangalia jinsi Yesu anavyochangamana na anavyozungumza kuhusu Wasamaria moja kwa moja ni kukabiliana na utamaduni: anawaadhibu wanafunzi wake kwa kukasirika wanapodharauliwa na wanakijiji Wasamaria (Luka 9:51-56); mfano wake mashuhuri una Msamaria kama shujaa na mmoja wa kuigwa (Luka 10:25-37); anakaa na kushirikishana kinywaji na mwanamke Msamaria (Yohana 4:1-38). Katika mifano hii yote, watazamaji Wayahudi wanakashfiwa. Kwetu leo, tunatakiwa kujiuliza wenyewe, Yesu alikuwa anafanya nini hapa?
Tunapomtazama Yesu na alivyojihusisha na Wasamaria kupitia kwa kioo cha ukarimu, tunaanza kuona kitu ambacho sio cha kawaida. Katika hamu yake ya kujifunua kwa mtu mwingine, anakuwa tayari kuachana na mkataba – anafanya zoezi la ukaribu na wale wasio ‘wasafi’, anashirikiana kwenye meza yake na ‘watu wa nje’ , naye anamtambua Mungu kazini ndani ya ‘asiye mwamini’. Kwa sababu ya hili, maadui wanakuwa majirani, wageni wanaonekana kuwa kama zawadi, na ‘mwingine’ anakuwa wakala wa neema ya Mungu.
Mfano wa ukarimu wa Yesu vile vile unatuita tufungue mioyo yetu kwa njia maalum kwa ajili ya wengine, bila kujali ni akina nani. Katika kufanya hivyo, tunaweza kutarajia nafasi takatifu kujifunua inayoruhusu neema ya Mungu kutiririka kupitia kwa Roho Mtakatifu. Hapa basi, patakuwa ni mahali pa mabadiliko.
Kwa ajili ya kutafakari:
Unaweza kufikiria kuhusu wakati wa kutoa ukarimu bila masharti kulikotoa nafasi ya neema ya Mungu kutiririka? Nini kilitokea?
Maombi kwa ajili ya leo:
Mpendwa Bwana, asante kutuonyesha jinsi ukarimu unavyofanana. Tusaidie tufungue mioyo yetu kwa wengine kwa njia maalum na kwa kufanya hivyo, tutengeneze nafasi kwa ajili ya neema kutiririka. Amina.
Kuhusu Mpango huu
Tukiwa na milango iliyofunguliwa na mioyo iliyofunguliwa, tunaweza kuwakaribisha wengine mahali watakapoonekana, wanapopendwa na pale wanapothaminiwa. Katika mfululizo huu wa siku nane, tunakualika uangalie kwa karibu mifano na hadithi za ukarimu zinazopatikana katika Biblia na uwe na muda wa kutafakari jinsi wewe unavyoweza kufanya ukarimu vizuri kwa kutumia maisha yako mwenyewe.
More
Tungependa kumshukuru Salvation Army kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org