Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Fungua Milango. Fungua Mioyo.Mfano

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

SIKU 5 YA 8

Tendo la Haki.

Ukarimu ni tendo la haki ya ufalme; ndani yake mna kumwona mwingine na mahitaji yake na kuchukua hatua ya kutaka kujibu. Sio tu aweze kuishi bali aweze kustawi na apate amani (shalom).*

Haki ya Ufalme ni kuhusu kuwakaribisha wageni kuwa sehemu ya maisha yetu na sisi tuwe sehemu ya maisha yao. Wageni, wale ambao wanaweza kuwa tofauti na sisi katika njia nyingi, wale wanaotoka nchi nyingine au waliopitia maisha tofauti, utamaduni au lugha, wanaweza kuwa wagumu kwetu kuwakaribisha. Lakini kama tunataka kufuata mfano wa Yesu na kuheshimu amri ya Mungu, tunatakiwa tuwafikie wale ambao wanaweza kujisikia hawajakaribishwa duniani kwa kumbatio lenye joto la jamii linaloweza kuonyesha upendo wa Mungu, tukitambua kwamba chochote tufanyacho kwa ‘walio wadogo’, tunamtendea Bwana (Mathayo 25:40). Hii inaweza kuhusisha matendo ya ukarimu wa asili kama kushirikiana chakula – lakini ni zaidi.

Katika Mambo ya Walawi 19:33–34, Mungu anatoa mwongozo wa wazi kwamba tusiwadhulumu wageni wanaoishi katika nchi yetu, bali tuwatendee kama wenyeji, tuwapende kama tujipendavyo sisi wenyewe. Tuwape ‘makazi’.

Makazi sio mahali, ni mahusiano.

Sio rahisi kuwa mgeni – bila kujua mwenendo gani ni wa kawaida, vazi lipi linakubalika au namna ya kuendesha majukumu ya maisha ya kila siku.

Kama wafuasi wa Yesu, tunatakiwa kuonyesha upendo na uvumilivu kwa mgeni aliye katikati yetu. Kwa yule anayehesabu taratibu fedha asizozizoea kwenye meza ya fedha, kwa yule mwenye mabegi mazito anayehitaji muda wa ziada kidogo apite kwenye eneo la usalama uwanja wa ndege, kwa yule anayesema maneno machache yasiyo sawa katika lugha ya kigeni. Tunatakiwa kuwakaribisha kwa upendo na kuwapa ‘makazi’ pamoja nasi.

Hii ni haki ya ufalme katika hali yake bora kabisa – kuishi sawa na kuweka sawa yaliyokosewa.

Kwa ajili ya kutafakari:

Namkaribisha namna gani mgeni katikati yangu (ujirani, shuleni, katika jamii)?

Ni kwa njia gani Mungu hujifunua kwangu kupitia kwa mgeni?

Maombi kwa ajili ya siku ya leo:

Mpendwa Bwana, tusaidie tumwone mgeni kupitia kwa macho yako. Twaomba utuonyeshe upendo na uvumilivu tunapojitahidi kujenga mahusiano nao.

* ‘Shalom’ ni neno la Kiebrania na salaam ya Kiyahudi, mara nyingi linatafsiriwa ‘amani’ linaloelezea ukamilifu na haki. Maana yake ni kuungana na wengine. Na uumbaji. Na Mungu.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

Tukiwa na milango iliyofunguliwa na mioyo iliyofunguliwa, tunaweza kuwakaribisha wengine mahali watakapoonekana, wanapopendwa na pale wanapothaminiwa. Katika mfululizo huu wa siku nane, tunakualika uangalie kwa karibu mifano na hadithi za ukarimu zinazopatikana katika Biblia na uwe na muda wa kutafakari jinsi wewe unavyoweza kufanya ukarimu vizuri kwa kutumia maisha yako mwenyewe.

More

Tungependa kumshukuru Salvation Army kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org